Yanga na Simba kukutana Septemba 16 Ngao ya Jamii

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuwa mchezo wa Ngao ya Jamii kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2025/26 utapigwa Septemba 16, 2025 jijinio Dar es Salaam.

Katika taarifa iliyoptolewa na Shirikisho hilo  Agosti 20 mwaka huu mesema mchezo huo utawahuisisha mabingwa wa Ligi Kuu Bara 2024/25 klabu ya Yanga dhidi ya mshindi wa pili wa ligi Simba SC.

Taarifa imeeleza kuwa mfumo wa mashindano hayo hautahusisha tena timu nne kama ilivyokuwa msimu uliopita bali timu mbili tu kutokana marekebisho ya kanuni yaliyopitishwa katika kikao kilichopita cha Kamati ya Utendaji ya TFF.

“Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuzindua msimu mpya wa mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kati ya Young Africans na Simba itachezwa tarehe 16 Septemba 2025 jijini Dar es Salaam”.

“Mfumo wa mashindano ya Ngao ya Jamii umebadilika kutokana na marekebisho ya Kanuni yaliyopitishwa katika kikao kilichopita cha Kamati ya Utendaji ya TFF”.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii