Kundi D kweye mashindano ya CHAN ambalo linajumuisha nchi za Kongo Brazaville, Sudan kasikazini, Nigeria pamoja na Senegal limekuwa kundi gumu baada ya timu hizo kuwa na pointi zinazokaribiana kasoro nchi ya Nigeria ambayo tayari wameshatolewa wakiwa hawajashinda wala kutoa sare mechi yoyote.
Timu ambazo Zina nafasi ya kufuzu kwenda robo fainali ni Sudan, Senegal na Kongo, kitu ambacho kinavutia kwenye mechi za leo ambazo ndiyo mechi za mwisho za kundi hilo zinakutanisha Sudan dhidi ya Senegal timu hizi mbili zote Zina point 4 na mechi nyingine ni Kongo dhidi ya Nigeria , Kongo ana point 2 ambazo amezipata kwa kutoa sare na Sudan na Senegal, wakati Nigeria ana pointi 0.