NEC " Hakuna sheria inayoruhusu kura kupigwa mapema "

Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema hakuna sheria inayoruhusu kura za mapema kupigwa kwa upande wa Tanzania bara katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Kura hiyo ni ile ambayo itapigwa Zanzibar na baadhi ya watu, ambazo siku ya uchaguzi watakuwa na majukumu ya kusimamia uchaguzi mkuu huo.

Kauli hiyo meelezwa na Mwenyekiti wa INEC Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Jackobs Mwambegele, wakati akizungumza na Wahariri wa vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam.

Amesema Zanzibar ilipitisha sheria ya kuruhusu upigwaji huo wa kura.

Mbali ya Hilo Jaji Mwambegele amesema raia wa Tanzania wanaoishi nje ya nchi hawataweza kupigakura kutokana na sheria kutaka zoezi kufanyika hapahapa nchini.

Tume huru ya taifa ya uchaguzi (INEC) inaendelea kukutana na makundi mbalimbali kuelezea maandalizi ya uchaguzi mkuu yalipofikia.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii