Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara limesema limemkamata Anastanzia Exavery Mahatane (27), maarufu Ebitoke katika fukwe za Msanga Mkuu Mjini Mtwara akiwa katika hali inayoonekana kuwa amechanganyikiwa na wala hakuwa ametumbukizwa katika shimo wala kutekwa kama ambavyo alivyokuwa ameeleza mitandaoni ambapo Polisi hao wamempeleka Ebitoke Hospitali ya Mkoa Mtwara kwa matibabu na limeomba Ndugu zake wafike Mtwara kumchukua.
Akiongea leo AAugust mosi mwaka huu Kamanda wa Polisi Mtwara Issa Suleiman amesema ““Mnamo July 30, 2025 Anastanzia Exavery Mahatane (27), maarufu Ebitoke ambaye ni Msanii wa comedy hapa Tanzania, Mkazi wa Dar es salaam, ambaye kwa sasa anaishi katika Kata na Kijiji cha Msanga Mkuu Wilaya ya Mtwara alichapisha taarifa katika akaunti zake za mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram kuwa yeye kwa sasa yupo Mtwara na kwamba ametumbukizwa katika shimo huko katika fukwe za Msanga Mkuu na kwamba wapo Watu ambao aliwataja kwa majina kuwa wanataka kumuua”
“Kwakuwa Jeshi la Polisi jukumu lake la msingi ni kulinda raia na mali zao, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara lilianza uchunguzi wa haraka sana ilikujua ukweli wa taarifa iliyotolewa na Anastanzia Mahatane, katika uchunguzi wa awali Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limebaini kwamba Ebitoke alifika Mtwara tangu
Aprili 2025 na kufikia katika hoteli moja iliyopo Msanga Mkuu na kuomba hifadhi kwa Watu waliokuwa wanafahamiana kabla ya maisha yake kumuendea vibaya huko alikokuwa”
“July 31, 2025 saa 11:00 jioni Jeshi la Polisi Mtwara lilimkamata Ebitoke huko katika fukwe za Msanga Mkuu akiwa katika hali inayoonekana kuwa amechanganyikiwa na wala hakuwa
ametumbukizwa katika shimo wala kutekwa kama ambavyo alivyokuwa ameeleza katika mitandao hiyo ya kijamii, Ebitoke amefikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya matibabu na Jeshi la Polisi Mtwara linawaomba ndugu na jamaa wa Ebitoke kufika Mkoa wa Mtwara kutoa msaada au kumchukua ndugu yao”