Mwanaume mwenye umri unaokadiriwa (25-30) ambaye hajafahamika jina wala makazi yake, amekutwa amefariki dunia kwenye dimbwi la maji linalotumika kumwagilia mbogamboga kwenye bustani katika Mtaa wa Malunga wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea tukio hilo na kudai kuwa uchunguzi bado unafanyika kubaini chanzo cha tukio hilo na kuwataka wananchi kuendelea kufika kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Manispaa ya Kahama kumtambua mtu huyo.
Kadhalika Kamanda magomi amewataka wananchi mkoani humo kufukia madimbwi na mashimo ambayo ni hatarishi yaliyoko katika maeneo wanamoishi ili kudhibiti majanga yakiwemo ya watu kutumbukia na kupoteza maisha.
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii