Sean Diddy aomba kuachiliwa kwa dhamana ya Bil 132

Mwanamuziki na mfanyabiashara maarufu Sean "Diddy" Combs anataka kuondolewa katika gereza la MDC Brooklyn, akidai kuwa mazingira ya gerezani ni kama "jahannamu." Kupitia mawakili wake Marc Agnifilo na Teny Geragos, Diddy ameomba tena kupewa dhamana ya dola Milioni 50 sawa na Tsh Bilioni 132 akisubiri hukumu yake inayotarajiwa mwezi Oktoba.

Katika ombi jipya lililowasilishwa mahakamani, mawakili wake wamesisitiza kuwa Diddy hastahili kuwekwa mahabusu kwa kosa ambalo, kwa mujibu wao, mara nyingi washitakiwa wengine huwa wanaruhusiwa kubaki huru hadi siku ya hukumu. 

Diddy anakabiliwa na mashtaka chini ya Mann Act, sheria ya mwaka 1910 inayohusiana na kusafirisha watu kwa madhumuni ya ngono.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii