Mchezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona yang'atwa na mbwa kwenye sehemu zake za siri.

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania Carles Perez ,

ambaye anakipiga kwenye klabu ya Aris Thessaloniki ya nchini Ugiriki ,amelazwa hospitalini baada ya kung'atwa na mbwa kwenye sehemu zake za siri.

Inaripotiwa nyota huyo hayupo katika hali mbaya sana lakini anaweza kufanyiwa upasuaji baada ya kushonwa nyuzi zaidi ya sita ili kuziba jeraha lake hilo.

Tukio hilo liliripotiwa siku ya jumatano ya July 30,na vyombo mbalimbali vya habari nchini Ugiriki na chanzo kikitajwa ni baada ya mchezaji huyo kufanya Jaribio la kuwatenganisha mbwa wawili waliokuwa wanapigana ndipo wakamjeruhi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii