RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa serikali yake itaanza kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa zinazoingizwa kutoka India, kuanzia Ijumaa ijayo.
Akizungumza kupitia mtandao wake wa Truth Social, Trump amesema hatua hiyo inatokana na uamuzi wa India kununua mafuta kutoka Urusi, hali inayokiuka vikwazo vya kimataifa. SOMA: Marekani Yaendeleza Diplomasia Asia
Hata hivyo, Trump alisisitiza kuwa majadiliano ya kibiashara kati ya Marekani na India bado yanaendelea. Serikali ya India imesema inachukulia kwa tahadhari kubwa uamuzi huo wa Marekani, huku ikieleza kuwa itaendelea kulinda maslahi ya taifa lake.