Rapa maarufu Eve ameweka wazi mtazamo wake kuhusu mabadiliko ya muziki wa rap nchini Uingereza, akisema kuwa kwa sasa rap ya U.K. imejipata na imepata sauti yake tofauti na ilivyokuwa zamani.
Amesema hayo akizungumza na chanzo kimoja cha habari akiwa katika ziara zake, ambapo alisisitiza kuwa Marekani bado ndiyo blueprint ya hip hop, ikiwa na historia ndefu na ushawishi mkubwa duniani. Hata hivyo, aliongeza kuwa U.K. kwa sasa iko kwenye nafasi nzuri ndani ya muziki wa hip hop na anafurahia mwelekeo huo.
Kwa mujibu wa Eve, mabadiliko haya yanaonyesha ukuaji wa hip hop kimataifa na jinsi kila eneo linavyoweza kuleta ladha yake ya kipekee kwenye mdundo.