DK. BALAFU AACHIA LYRICS VIDEO YA “NEVER SELL MY SOUL”

Msanii anayechipukia kwa kasi, Dk. Balafu, ameendelea kutikisa anga ya muziki baada ya kuachia lyrics video ya wimbo wake mpya “Never Sell My Soul”. Audio ya wimbo huu, iliyotoka wiki chache zilizopita, imepokelewa vizuri sana na mashabiki kutokana na ujumbe wake wa kuhamasisha uthubutu, uaminifu kwa nafsi, na kutokubali kushawishiwa kufanya maamuzi yanayokwenda kinyume na misimamo binafsi.

Kupitia lyrics video hii, mashabiki wanapata nafasi ya kufuatilia maneno ya wimbo kwa ukaribu zaidi na kuelewa ujumbe wa kina alioukusudia. “Never Sell My Soul” inaendelea kujipatia mashabiki wapya na kuimarisha nafasi ya Dk. Balafu katika muziki wa kizazi kipya.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii