Magenge ya wahalifu yamewaua maafisa 13 wa usalama, wakiwemo polisi wawili na walinzi 11, katika jimbo la Zamfara kaskazini Magharibi mwa Nigeria katika ghasia za hivi punde katika eneo hilo, vyanzo vya habari vimeripot.
Majambazi walivamia kijiji cha Adabka wilayani Bukkuyum siku ya Ijumaa na kuwateka nyara baadhi ya wakaazi.
Majambazi hao kisha waliwafyatulia risasi polisi na walinzi waliokuwa wakiwafuata ili kuokoa mateka.
Mbunge wa eneo hilo Hamisu Faru, amesema hawajachukua miili ya watu waliouawa kutokana na hofu ya mashambulio zaidi kutoka kwa magenge hayo yanayokaa msituni.
Vyanzo vya habari vinasema wakaazi wengi wamekimbia kijiji hicho kwa kuhofia mashambulio mapya.
Magenge ya wahalifu kwa miaka mingi wamekuwa wakihangaisha jamii za kaskazini-magharibi na katikati mwa Nigeria, kuvamia vijiji, kuwateka nyara wakazi, kupora na kisha kuchoma nyumba.