Ahukumiwa miaka 30 jera kwa kosa kulawiti mtoto

Mahakama ya Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, imemhukumu Kulwa Said Omary (26) mkazi wa Bungu "A" kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka (3) (jina limehifadhiwa).


Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Mhe. Talsila John Kisoka, ambapo amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo Aprili 1, 2025 huko Bungu "A" wilayani Kibiti.

Upande wa mashtaka ulikuwa na jumla ya mashahidi sita akiwemo muathirika mwenyewe pamoja na daktari wa binadamu, ambapo mashahidi wote kwa pamoja waliwasilisha ushahidi wao na mahakama kuthibitisha kosa pasi na shaka na kumtia hatiani mtuhumiwa.

Mshtakiwa katika utetezi wake aliomba mahakama impunguzie adhabu kwani ni kosa lake la kwanza, ambapo mahakama ilitupilia mbali utetezi wake na kumuhukumu mshtakiwa kifungo cha miaka 30.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii