Mawaziri wawili nchini Ghana wafariki wa helikopta

Watu  wanne wafariki dunia kwa ajali ya helikopta iliyotokea August 6 mwaka huu katika eneo la Ashanti nchini Ghana na kusababisha vifo vya watu wanane huku miongoni mwao kuna mawaziri wawili.

Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali ya Ghana, watu wote wanane waliokuwamo kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia huku miongoni mwao ni Waziri wa Ulinzi, Edward Boamah na Waziri wa Mazingira Ibrahim Murtala.

Kituo cha televisheni cha Joy News kilionyesha mkanda wa video iliyorekodiwa na simu kutoka eneo la ajali ikionyesha mabaki ya ndege yakiwaka moto na kufuka moshi katika eneo la msitu mkubwa mapema jana.

Wengine ni Mohammad Limuna, Naibu Mratibu wa Usalama wa Kitaifa na waziri wa zamani wa kilimo na Samuel Sarpong, makamu mwenyekiti wa Chama cha National Democratic Congress (NDC).

Katika ajali hiyo, Jeshi la Wananchi wa Ghana liliripoti mapema Jumatano kuwa helikopta ya Jeshi la Anga ilitoweka kwenye rada muda mfupi baada ya kupaa kutoka Accra saa 3:00 asubuhi kwa saa za Ghana (09:00 GMT), ikielekea mji wa Obuasi, kaskazini-magharibi mwa mji mkuu.

Taarifa hiyo ilieleza kulikuwa na wahudumu watatu na abiria watano ndani ya ndege hiyo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii