Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, ameikabidhi Taifa Stars kiasi cha Sh milioni 10 za goli la mama na kuungwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ambaye ametoa kiasi cha Sh milioni 20 pamoja na mdau wa michezo, Azzim Dewji, ambaye ameahidi kiasi cha Sh milioni 25 kwa timu hiyo.
Stars imejinyakulia fedha hizo baada ya ushindi wa goli 1 - 0, dhidi ya Mauritania, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, Agosti 06, 2025.