Mashindano ya Kwanza ya Dunia ya Soka la Roboti Kuandaliwa , Timu 30 Kuonesha Ubora wa AI

Timu 30 kutoka mataifa kama Marekani, Brazil, Ujerumani na Ureno zinajiandaa kwa mashindano ya kwanza ya dunia ya roboti, ambapo roboti hao wenye akili bandia (AI) watashiriki kwenye mechi za soka za wachezaji watano kwa upande mmoja bila msaada wa binadamu. Timu ya Shanhai kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha China ambao walikuwa washindi wa pili kwenye RoboCup mwezi Juni huko Brazil  walionekana wakifanya mazoezi Jumatatu.

Roboti hao wenye sensa za kuona wana uwezo wa kuona mpira, kutembea, na kujirekebisha wanapoanguka  yote kwa kutumia AI. Ingawa roboti wengi wametengenezwa China, kila timu imeandika mfumo wake wa maamuzi kwa roboti wake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii