Idadi ya vifo kutokana na ajali ya ajali ya ndege ya kivita ya Jeshi la Wanahewa la Bangladesh katika shule huko Dhaka Jumatatu, Julai 21, imeongezeka na kufikia angalau 27, wengi wao wakiwa wanafunzi, afisa wa Wizara ya Afya ametangaza leo Jumanne.
"Kwa wakati huu, watu 27 ndio inasadikiwa kuwa wamefariki, ikiwa ni pamoja na watoto 25 na rubani," Saydur Rahman amewaambia waandishi wa habari, akiongeza kuwa watu 78 waliojeruhiwa wanasalia hospitalini siku moja baada ya ajali.
Kati ya takriban majeruhi 170 waliorekodiwa na idara ya huduma za dharura saa chache baada ya ajali hiyo, "78 bado wanatibiwa katika hospitali mbalimbali" katika mji mkuu, ameongeza Saydur Rahman. Wengi wao wanatibiwa katika idara ya dharura ya Taasisi ya Kitaifa ya Maeraha ya Kuungua kwa Moto huko Dhaka.
Kulingana na jeshi, ndege hiyo aina ya F-7 BGI iliyotengenezwa na China, ilipata tatizo la kiufundi na kuanguka mapema siku ya Jumatatu alasiri katika eneo la shule ya Milestone kaskazini magharibi mwa Dhaka.
Maafa haya yaliyosababishwa na ndege hiyo ndiyo mabaya zaidi kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa nchini Bangladeshi, ambayo inafanya maombolezo ya kitaifa leo Jumanne.
Ndege hiyo yenye injini moja, ambayo ilikuwa imepaa dakika chache mapema kutoka kituo cha anga nje kidogo ya mji wa Dhaka, iligonga jengo la ghorofa mbili ambapo kulikuwa kukitolewa visomo mbalimali, ambalo mara moja liliwaka moto.
Siku moja baada ya ajali hiyo, shule ya Milestone, ambayo kwa kawaida ina wanafunzi wapatao 7,000, lakini siku hiyo shule haikua na wanafunzi wakati ajali inatokea.
Mkuu wa serikali ya mpito ya Bangladesh, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Muhammad Yunus, alitangaza Jumanne kuwa siku ya maombolezo ya kitaifa.