Klabu ya Yanga SC imethibitisha rasmi kumuongezea kiungo wao mahiri, Mudathir Yahya, mkataba mpya wa miaka miwili ikiwa hatua hiyo inamaanisha kuwa nyota huyo ataendelea kuitumikia klabu hiyo ya Jangwani hadi mwaka 2027.
Mudathir ambaye ni miongoni mwa wachezaji waandamizi ndani ya kikosi cha Yanga, amepewa mkataba huo kama sehemu ya mpango wa klabu kuimarisha kikosi chao kuelekea mashindano ya ndani na ya kimataifa kwa misimu ijayo.