Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wamepiga hatua nyingine kubwa kwenye dirisha la usajili baada ya kufanikiwa kumnasa kiungo wa CS Sfaxien ya Tunisia, Mussa Balla Conte (21).
Conte, ambaye pia alikuwa akiwindwa vikali na watani wa jadi, Simba SC, aliwasili nchini leo asubuhi akitokea Tunisia na kupokelewa na baadhi ya viongozi wa Yanga jijini Dar es Salaam.