Lamine Yamal akabidhiwa jezi namba 10 ya Messi Barcelona, asaini Mkataba mpya mpaka 2031

Kinda mahiri wa FC Barcelona, Lamine Yamal, amesaini mkataba mpya wa muda mrefu na klabu hiyo, ambao utamuweka Camp Nou hadi tarehe 30 Juni 2031 amekabidhiwa rasmi jezi namba 10, namba yenye heshima kubwa katika historia ya klabu hiyo.

Jezi hiyo imewahi kuvaliwa na vigogo wa soka kama Ronaldinho Gaucho, Lionel Messi, na hivi karibuni Ansu Fati, na sasa ni zamu ya Yamal kuibeba, ishara ya imani kubwa ya klabu kwake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii