Msanii maarufu wa muziki kutoka Nigeria, David Adedeji Adeleke, anayefahamika zaidi kwa jina la Davido, ameendelea kuthibitisha kuwa ni mmoja wa mastaa matajiri zaidi barani Afrika baada ya kununua gari jipya aina ya Lamborghini Revuelto.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, Davido amenunua gari hilo la kifahari kwa gharama ya zaidi ya Dola Milioni 1 sawa na takribani Shilingi Bilioni 2.6 za Kitanzania.