Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Jux, kwa mara nyingine amewashangaza mashabiki wake baada ya kuweka wazi kuwa yeye na mpenzi wake Priscilla wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza. Taarifa hizo zilitolewa kupitia Picha za kipekee ziliyosambaa mitandaoni, ikionyesha picha za ujauzito wa Priscilla huku Jux akionekana mwenye furaha na shukrani.
Katika kusherehekea hatua hiyo mpya ya maisha, Jux pia aliachia rasmi wimbo mpya unaoitwa “Thank You”, ambao ni wa aina ya Afro-RnB ukiwa umejaa ujumbe wa upendo, shukrani na matumaini. Wimbo huo unaonyesha upande wa kihisia wa msanii huyo na ni wazi kuwa umetokana na hisia halisi kutoka kwenye maisha yake binafsi.
Mashabiki na watu maarufu mbalimbali wameendelea kuwapongeza kwa hatua hiyo ya kipekee, huku wengi wakisifu uamuzi wa Jux kutumia sanaa kuonyesha furaha ya kuwa baba. Wimbo “Thank You” tayari unapatikana kwenye majukwaa yote ya muziki na umepokelewa vyema na mashabiki ndani na nje ya Tanzania.