Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi Romain Folz kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa 2025–2026.
Folz (35) mwenye leseni za UEFA Pro na CONMEBOL Pro, ataliongoza benchi la Yanga msimu ujao huku wananchi wakitarajia kuendeleza mafanikio ambayo wamekuwa wakipata kwa misimu minne mfululizo.
Folz anachukua nafasi ya Miloud Hamdi aliyetimkia Ismaily ya Misri baada ya kuitumikia Yanga kwa takriban miezi sita na kuifanikisha kushinda ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la Muungano na Kombe la FA msimu uliopita.