Klabu ya Arsenal mbioni kufanikisha azma yake ya muda mrefu, ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji hatari kutoka Sweden, Viktor Gyökeres, kutoka klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Arsenal italipa euro milioni 63.5 kama ada ya awali, sawa na takribani shilingi za Kitanzania bilioni 260, na kuongeza euro milioni 10 (zaidi ya TSh bilioni 41) kama bonasi kulingana na mafanikio yake. Aidha, mawakala wake wamekubali kupunguza malipo yao ili kusaidia kufanikisha dili hilo.
Gyökeres, ambaye alifunga magoli 43 msimu uliopita katika michuano yote, sasa atavaa jezi ya Arsenal kwa mkataba wa miaka mitano. Usajili huu unaelezwa kuwa ni wa “kusisimua mno” kwa kocha Mikel Arteta, ambaye alikuwa akitafuta mshambuliaji mwenye nguvu, kasi na uwezo wa kufunga.
“Huyu ni mchezaji tuliyemfuatilia kwa muda mrefu. Ana kila kitu tunachohitaji mbele,” alisema Arteta kwa kifupi.