Kamati ya Uchaguzi TFF Yamwacha Karia Pekee Urais 2025

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewatangaza rasmi wagombea watano wa nafasi ya urais kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho, na kumwacha Wallace Karia kama mgombea pekee aliyeendelea baada ya usaili.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Kiomoni Kibamba, imeelezwa kuwa ni Karia pekee aliyekidhi vigezo kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za TFF.

“Wallace Karia ndiye mgombea pekee aliyekidhi vigezo vya kugombea nafasi ya urais wa TFF. Wagombea wengine watano hawakufikia masharti yanayohitajika,” alisema Kibamba wakati akisoma ripoti ya usaili.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii