Simba Yawaita Yanga Kuwasapoti CAF

mchezo wao wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas kutoka Ivory Coast, unaotarajiwa kufanyika Februari 13, katika Uwanja wa Mkapa, Dar.
Simba inatarajiwa kucheza mchezo huo
ambao ni wa kwanza wa Kundi D ambapo timu nyingine ambazo zipo katika kundi hilo ni RS Berkane ya Morocco na Union Sportive Gerndamarie ya nchini Niger.


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba,AhmedAlly, alisema: “Nawakaribisha mashabiki wa timu zote kuja kutushangilia, sio tu mashabiki wa Simba japo naamini kuwa Simba tuna mashabiki wengi sana ambao wangetosha kuja lakini hata wale wengine pia mnakaribishwa kuja kutushangilia.

“Kwetu michuano ya kimataifa si jambo geni na tumezoea kushiriki, safari hii tunahitaji kuona tunafika mbali katika michuano hii, hivyo tumejipanga kupambana katika mchezo huo kuhakikisha kuwa tunafikia malengo yetu katika michuano hii mikubwa baraniAfrika.”


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii