Zitto akamatwa na kuachiliwa kwa dhamana

Chama cha ACTWazalendo kimetoa taarifa kuwa Kiongozi mstaafu wa chama hicho Zitto Kabwe, alishikiliwa na Jeshi la Polisi, Saa Sita Usiku, Julai 14 mwaka huu baada ya kuvamiwa akiwa hotelini, baadaye alipelekwa Kituo cha Polisi akazuiwa kwa zaidi ya dakika 30 bila kuelezwa kosa lake mara moja.

ACT imeeleza baada ya majibizano ya muda mrefu Askari walisema wanamshikilia kwa kosa la kutoa kauli za vitisho alivyotoa wakati wa hotuba yake ya Julai 10 mwaka huu kwenye mkutano wa hadhara Tunduru Kaskazini, ambapo chama kimeeleza aliachiwa Saa Nane Usiku bila masharti.

Ikumbukwe Zitto alinukuliwa akisema Askari yeyote au Watendaji wa Serikali watakaojihusisha na Kura Bandia wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 basi mhusika au Wahusika “watakuwa halali yao”


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii