Hali ya Joel Lwaga Kiafya Sio Nzuri

Joel Lwaga amefunguka kuhusu hali yake ya kiafya baada ya kupata ajali ya kimichezo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lwaga ameeleza kuwa alipata jeraha la mguu wakati akicheza soka.


Katika ujumbe wake, aliandika, "Kwa wale mmekuwa mkiniuliza shida ni nini, nilipata ajali ya kimichezo nikiwa mpirani (soccer) nikachanika nyama za paja kwa ndani (hamstring) ama misuli ya nyuma ya paja."


Muimbaji huyo wa Olodumale alifafanua kuwa amekuwa akipokea matibabu kwa muda wa wiki mbili sasa katika Hospitali ya Aga Khan na anaendelea vizuri chini ya uangalizi wa madaktari bingwa. Kwa sasa, ameshauriwa kupumzika ili kuruhusu kidonda chake kipone kikamilifu.


Alimalizia kwa kuwashukuru mashabiki na wafuasi wake wote kwa maombi na salaam za kumtakia afueni ya haraka.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii