Kocha wa klabu ya Yanga Sc, Miloud Hamdi amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Juni wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2024/2025 akiwashinda Rachid Taoussi wa Azam FC na Fred Felix wa Pamba Jiji alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za TFF.
Kocha huyo raia wa Algeria ambaye kwa sasa amejiunga na klabu ya Ismaily ya Misri aliiongoza Yanga kushinda michezo yote mitatu iliyocheza mwezi huo na kutwaa ubingwa wa wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2024/2025. Yanga ilizifunga Tanzania Prisons (0-5), Dodoma Jiji (5-0) na Simba (2-0)