Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kocha wa kikosi hicho Fadlu Davids anahusika moja kwa moja na kutoongezwa au kuvunjwa kwa mikataba kwa baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo wakati huu ambao wanajiimarisha kuelekea msimu ujao
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ahmed amesema wachezaji walioondoka hadi sasa ambao ni mlinda lango Aishi Manula aliyerejea Azam FC, Valentin Nouma na kiungo Fabrice ngoma ambao licha ya kutokuwa na taarifa kutoka klabuni hapo wameaga kupitia mitandao yao ya kijamii ni kwa maoni ya kocha Fadlu
“Labda tu niseme ya kwamba chochote unachokiona ndani ya Simba kinachohusiana na wachezaji ni maoni, melekezo, mapendekezo, maelekezo na mawazo ya mwalimu wetu Fadlu Davids.
Mwalimu ndiye anayetoa mapendekezo ya nani aletwe nani aachwe nani auzwe na nani aongezewe mkataba ni maelekezo ya kocha Fadlu.