Fadlu Davids" Tutaboresha Kikosi Simba Kwa Msimu Ujao"

Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids, amesema kuwa kikosi hicho kinahitaji maboresho baada ya kumaliza msimu wa Ligi Kuu Bara kikiwa nafasi ya pili kwa alama 78, nyuma ya mabingwa Yanga SC waliomaliza na pointi 82.

Simba SC ilipoteza mechi zote mbili za Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC msimu huu—mzunguko wa kwanza na wa pili—na kupoteza jumla ya pointi sita huku ikiruhusu mabao matatu bila kufunga hata moja kwenye michezo hiyo miwili ya hadhi kubwa.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa msimu, Kocha Fadlu alisema:

“Tutafanyia kazi makosa ambayo yametokea na kuboresha kikosi kwa ajili ya wakati ujao. Bado wachezaji ni vijana na wamepambana kufika hapa tulipo.”

Kocha huyo ameweka wazi kuwa pamoja na changamoto zilizojitokeza, bado ana imani na kikosi chake na anatarajia kuboresha safu mbalimbali kuelekea msimu ujao ili kuwania tena taji la Ligi Kuu pamoja na kufanya vizuri kimataifa.

Mashabiki wa Simba SC wanatarajia kuona usajili wa wachezaji wapya na maamuzi ya kiufundi yatakayorejesha heshima ya klabu hiyo msimu ujao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii