Wapalestina 56 wauawa Gaza

 IDARA ya Ulinzi wa Raia katika Ukanda wa Gaza imethibitisha kuwa watu 56 wameuawa  Juni 26, 2025 kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la Israel katika maeneo mbalimbali ya ukanda huo.

Taarifa ya msemaji wa idara hiyo, Mahmud Bassal, imeeleza kuwa mashambulizi hayo yalilenga maeneo tofauti ya Gaza na kusababisha vifo vya raia, wakiwemo watu sita waliokuwa wakisubiri msaada wa kibinadamu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez, amesema kinachoendelea Gaza ni mauaji ya halaiki na kutoa wito kwa Umoja wa Ulaya kusitisha mara moja mkataba wake wa ushirikiano na Israel.

Mashambulizi ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza yalianza baada ya shambulio la Oktoba 7, 2023 lililofanywa na kundi la Hamas, ambapo watu 1,219 waliuawa nchini Israel. Tangu kipindi hicho, jumla ya Wapalestina waliouawa imefikia zaidi ya 56,000, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza inayoongozwa na kundi la Hamas.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii