Magenge ya uhalifu yatikisa Haiti ongezeko la vitendo vya ukatili– UN

 WATAALAMU wa Umoja wa Mataifa wametahadharisha kuwa magenge ya wahalifu yanayodhibiti maeneo makubwa ya Haiti yameongeza vitendo vya ukatili ikiwemo mauaji, ubakaji na utekaji nyara.

Taarifa ya jopo la wataalamu wanaosimamia vikwazo dhidi ya magenge hayo imeeleza kuwa hali ya usalama inazidi kuzorota kutokana na udhaifu wa serikali ya mpito isiyo na rais wala bunge, huku jeshi la polisi likiwa limezidiwa na magenge yenye silaha nzito licha ya vikwazo.

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa licha ya kuwepo kwa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani, ambacho nacho kinakabiliwa na changamoto za kifedha na vifaa, bado hakuna mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kurejesha utulivu na utawala wa sheria nchini humo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii