Simba imethibitisha kucheza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Yanga ‘Kariakoo Derby leo d kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mechi hiyo imepangwa kuchezwa kuanzia saa 11:00 jioni ambapo Yanga itakuwa mwenyeji.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Simba imeweka tangazo la mechi hiyo na kuandika ‘Tutakuwepo’.
Mchezo huo wa leo una maana kubwa kwa timu zote mbili kwani ndio utatoa uamuzi wa ipi itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kutokana na utofauti wa pointi moja uliopo baina yao kwenye msimamo wa ligi.