Watanzania 42 waliokuwa wamekwama nchini Israel kwa sababu ya mapigano kati ya nchi hiyo na Iran watarejea nchini leo tarehe 25 Juni 2025, kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.
Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasilino ya serikali Watanzania hao watawasili nchini katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza litawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Unguja saa 6:55 mchana, na kundi la pili litawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam saa 11:55 jioni.
Kurejea kwa Watanzania hao ni matokeo ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Serikali kuhakikisha Watanzania hao wanarejea nyumbani salama. Wizara kupitia Balozi za Tanzania nchini Israel na Misri zimeratibu safari hiyo.
Serikali inawahakikishia wananchi kuwa itaendelea kuratibu safari hizo hadi Watanzania wote waliokwama katika mataifa hayo, wanarejeshwa nyumbani.