Vijana wenye hasira kali wachoma kituo cha polisi

VIJANA waliokuwa na hasira waliteketeza kituo cha polisi cha Mawego katika eneo la Rachuonyo Kaskazini wakati wa ibada ya mazishi ya mwalimu aliyeuawa, Albert Ojwang’.

Ambapo awali alikuwa amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Mawego baada ya kukamatwa na polisi nyumbani kwa wazazi wake katika Kijiji cha Kakoth, eneo la Kokwanyo, katika eneo la bunge jirani la Kabondo Kasipul.

Mipango ilikuwa imewekwa ili ibada ya mazishi ifanyike katika Shule ya Msingi ya Nyawango, ambapo masomo yalisitishwa ili kutoa nafasi kwa umati mkubwa wa waombolezaji.

Hata hivyo, mambo hayakwenda kama ilivyopangwa daada ya mwili kuwasili Lida, gari la kubeba maiti lenye kioo cha wazi kilichowawezesha waombolezaji kuona jeneza lililotarajiwa kuelekea moja kwa moja nyumbani kwa mwendazake.

Lakini vijana waliokuwa wameungana na wanafunzi kutoka Chuo cha Ufundi cha Mawego walifunga barabara na kusisitiza kuwa mwili upelekwe kwanza katika kituo cha polisi cha Mawego.

Baba wa marehemu, Bw Meshack Opiyo, alijaribu kuwaomba waombolezaji waruhusu familia kupeleka mwili moja kwa moja nyumbani  ambapo wakati huu  mkewe Eucabeth Adhiambo na mjane wa Ojwang’, Nevnina Onyango, walikuwa kwenye gari moja.

Bw Opiyo alisimama juu ya paa la gari huku akizungumza kwa kipaza sauti kilichounganishwa kwenye mfumo wa sauti uliokuwa kwenye lori lililokuwa sehemu ya msafara wa mazishi.

Ambapo Vijana walijitwika jukumu la kuutoa mwili kutoka kwenye gari la maiti na wakabeba jeneza kwa mikono yao, wakitembea takriban kilomita tatu hadi kituo cha Polisi cha Mawego.

Walipofika kituoni, baadhi yao walianza kurusha mawe wakilenga madirisha na  wakati huo, maafisa wa polisi waliokuwa kituoni humo walikuwa wamekimbia.

Baada ya kugundua kwamba polisi hawakuwepo, vijana walianza kuharibu mali Katika vurugu hizo, vijana walishusha bendera mbili – ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi na bendera ya taifa ikiwa Kundi moja lilirudisha mwili hadi Soko la Lida na kundi jingine likabaki kituoni kuchoma moto jengo la kituo.

Aidha jengo jingine la kudumu ambalo hutoa makazi kwa maafisa wa polisi pia lilitiwa moto, lakini maafisa wa polisi waliotumwa kutoka vituo mbalimbali waliwasili na kufanikiwa kuuzima.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii