Serikali Zanzibar yatoa mbinu kikosi cha polisi kukabiliana na wahalifu

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo imesema itahakikisha inawapatia kila aina ya nyezo kikosi cha Polisi Utalii ili kuhakikisha ufanisi wa utendaji kazi wa kikosi hicho katika kulinda watalii wanaokuja nchini.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Dkt Aboud Suleiman Jumbe wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya Polisi Utalii na Diplomasia yanayoendeshwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali ya Uingereza katika kusaidia kikosi hicho.

Amesema kwa kuwa sekta ya utalii ni sekta nyeti na muhimu kwa uchumi wa Zanzibar, serikali inaendelea kuchukua juhudi madhubuti za kuimarisha sekta hiyo Muhimu.

Kwa upande wa Mkuu wa Operesheni na Mafunzo Kamisheni wa Polisi Zanzibar Matias Nyange pamoja Mkuu wa Kikosi cha Utalii na Diplomasia Kepteni Saleh Juma Seif wamesema kwasasa hali ya usalama kwa watalii imeimarika kwani polisi hao hufanya doria katika maeneo yote ya fukwe na nchi kavu kuhakikisha usalama wa watalii unaimarishwa Zanzibar.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii