Wananchi wa Kijiji cha Kwanyange, Kata ya Kivisini, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro, wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya kutokana na ukosefu wa Zahanati katika kijiji chao,kufuatia uzinduzi wa zahanati mpya yenye thamani ya Shilingi milioni 169.2 iliyotekelezwa na Serikali.
Wakizungumza Julai mosi mwaka huu wakati wa uzinduzi wa zahanati hiyo, wananchi hao wameeza hapo awali walilazimika kutembea zaidi ya kilomita saba kufuata huduma za afya, hali iliyokuwa ikihatarisha afya zao hasa kina mama wajawazito na watoto.
Na kueleza kuwa Mazingira yao si rafiki kwani wanakumbwa na wanyama wakali, lakini sasa huduma za afya zikiwa karibu zitawasaidia sana hivyo wanaomba Serikali iwaangazie zaidi, kwa watupatia wataalamu wa afya pamoja na nyumba zao za kuishi.
Akisoma taarifa ya mradi huo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, dkt Serijo Kusekwa, amesema mradi ulianza kwa ushirikiano kati ya wananchi na kampuni ya Kifaru Quarrier hadi hatua ya lenta, na baadaye Serikali ikaukamilisha kupitia mapato ya ndani mwaka wa fedha 2024/2025.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ndg. Ismail Ali Ussi, mara baada ya kukaguaa mradi huo pamoja nyaraka za amesema wamejiridhisha na ubora wa kazi na matumizi ya fedha, na kuongeza kuwa tayari taarifa kuhusu uhitaji wa watumishi wa afya limewasilishwa serikalini.