Abdul Nondo atoa wito kwa wananchi kutosusia uchaguzi mkuu

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, Mwenyekiti wa Taifa wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo, Abdul Nondo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuzilinda kura zao kwa ajili ya kulinda demokrasia ya kweli.

Ametoa wito huo Julai mosi mwaka huu wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kalinzi, katika Jimbo la Kigoma Kaskazini.

Nondo amewahimiza wananchi kutojihusisha na ususiaji wa uchaguzi, akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuwapa mwanya baadhi ya vyama ambavyo tayari vimejiandaa kushiriki kikamilifu katika mchakato huo wa kidemokrasia.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii