Jobe Belligham kuukosa mchezo wa robo fainali dhidi ya Real Madrid

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Borrusia Dortmund Jobe Belligham,atakosekana kwenye mchezo wa robo fainali ya kombe la dunia la vilabu dhidi ya Real Madrid utakaopigwa kwenye dimba la Metlife nchini Marekani.

Jobe ataukosa mchezo huo baada ya kupewa adhabu ya kadi ya njano katika mchezo dhidi ya CF Monterrey uliopigwa usiku wa kuamkia leo na kumalizika kwa Dortmund kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.

Hii imepunguza ladha kwa baadhi ya mashabiki wengi wa soka duniani baada ya wengi kutamani mchezo huo ungepigwa kwa kushuhudia upinzani mkubwa kati ya kiungo huyo na kaka yake Jude Belligham anayekipiga Real Madrid .

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii