Mahakama ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela Mussa Hassan Ntakula (70), Mkazi wa Kijiji cha Ngalinje baada ya kupatikana na hatia ya kosa la udhalilishaji wa kingono ambapo hukumu hiyo imetolewa mbele ya Hakimu Mfawadhi wa Mahakama ya Wilaya ya Masasi, Rehema Iddi na mwendesha mashtaka Miraji Kajini.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mtwara Issa Suleiman amesema hayo leo June 27,2025 wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya Mahakamani kwa kipindi cha mwezi May, 2025 baada ya kuwakamata Watuhumiwa mbalimbali na baadhi ya Watuhumiwa kufikishwa Mahakamani.
Aidha mshtakiwa alitenda kosa hilo April 08,2025 katika Kijiji cha Ngalinje baada ya kumlaghai Mhanga Mwanafunzi wa darasa la sita (13) (jina la Shule limehifadhiwa) anayeishi naye Mtaa na Kijiji kimoja kwa kumwita nyumbani kisha kumvua nguo, kutoa sehemu zake za siri (uume) kisha kuchezesha kwenye nyeti za mtoto huyo”