Enock Bella ajitokeza kumuomba msamaha Mbosso

Msaniii Enock Bella amejitokeza hadharani kumuomba msamaha Mbosso kwa yote ambayo amemkosea katika maisha waliyoishi zamani mpaka sasa.

Enock ameomba msamaha huo baada ya Mbosso kuzungumza na waandishi wa habari kusema anasononeshwa na Enock anavyomzungumzia kwa watu.


"Sisi ni ndugu Mbosso wengi watahitaji kulitumia hili jambo kama fursa maana haya yote yalishapita. Nisamehe kwa kila nilipokukosea nakumbuka nilishawahi kukwambia before neno hili"

"Muziki uendelee undugu wetu hauwezi vunjika bro Room Number 3 ndio habari ya mjini" - Ameandika  Enock

Wawili hao wamewahi kuwa chini ya kundi la Yamoto Band ambalo lilifanya vizuri kwenye muziki wa BongoFlava.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii