Mambo matatu yaliyopelekea Gennaro kuwa kocha mkuu timu ya Italia

Shirikisho la Mpira wa Miguu Italia (FIGC) limetaja sifa tatu zilizoishawishi  iamue kumpa Gennaro Gattuso nafasi ya ukocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo ‘Azzuri’.
Uamuzi wa kumpa kibarua hicho Gattuso ulifikiwa muda mfupi baada ya Italia kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Norway katika mechi ya kundi I ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwakani kupitia kanda ya Ulaya.

FIGC imesema kuwa weledi, uwezo wa kuhamasisha na uzoefu ni sababu zilizowafanya wampe kazi hiyo Gattuso anayerithi mikoba ya Luciano Spalletti aliyetimuliwa.

Gattuso ni alama ya Mpira wa Miguu wa Italia. Jezi ya Bluu ni kama ngozi yake ya pili. Hamasa, weledi na uzoefu wake vitakuwa muhimu.

Italia haijafuzu fainali za Kombe la Dunia mara mbili tofauti zilizopita na harakati zao za kufuzu Fainali zijazo zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico, zilianza vibaya kwa kuchapwa mabao 3-0 na Norway, Wiki iliyopita.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii