Mwimbaji mashuhuri wa Kimataifa, Justin Bieber, ameonekana akijibizana vikali na paparazzi nje ya Soho House, Malibu, California usiku wa Alhamisi, tarehe 12 Juni. Tukio hilo lililodumu kwa takribani dakika 11 lilihusisha matusi mazito na mabishano ya moja kwa moja kati ya Bieber na wapiga picha waliokuwa wakimfuatilia.
Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lilianza baada ya timu ya usalama ya Bieber kuwaamuru wapiga picha hao waondoke karibu na gari lake. Hata hivyo, paparazzi hao waliendelea kurekodi, jambo lililompelekea mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kufoka.
“Si leo bro,” alisema Bieber huku akijifunika uso kwa mkono, kabla ya kuanza kupaza sauti:
“Unafikiri inakuwaje ukiwa usoni mwangu? Ondoka kwenye uso wangu!”
Bieber alionekana akiwa katika hali ya hasira na akasisitiza kuwa hana hofu ya kuweka mipaka kwa wapiga picha hao waliokuwa wakimuuliza maswali yanayohusiana na madai ya uwezekano wa kufukuzwa nchini kutokana na misako ya wahamiaji.
“Mimi ni mwanaume halisi mwenye familia halisi. Na nyinyi mpo usoni mwangu,” alisema kwa msisitizo.
“Leo hii, naweka mipaka kwa wote. Sitaki potovu zenu.”
Aliwatahadharisha kwamba wao si marafiki zake, na hivyo hawakuwa na haki ya kumuuliza maswali ya binafsi:
Kwa hasira na huzuni, Bieber alisema:
“Mimi ni baba, nina familia, na nyinyi mpo kwenye mali ya mtu binafsi mkiwa mbele ya gari langu.”
Wakati mmoja, paparazzi walimtakia Bieber Heri ya Siku ya Baba (Father’s Day), lakini alijibu kwa hasira:
“Sikujui. Huwezi kwenda kwa mtu usiyemfahamu na kuanza kusema mambo mbele ya kamera. Hilo halina maana kama mimi ni mtu maarufu au la.”
“Kama kawaida, mtachukua video hii na kuipotosha. Mnafikiria mimi ni mjinga? Mimi niko katika kikomo cha uvumilivu wangu.”
Akiendelea kuzungumza kwa hasira, aliongeza:
“Mnachanganya hasira yangu na ukosefu wa heshima. Lakini ukweli ni kwamba mnanikosea heshima, na sitakubali hilo.”
Bieber alisisitiza kuwa kazi za paparazzi ni kwa gharama ya maisha ya watu wengine, na kwamba kuchokozwa mara kwa mara kunaumiza moyo wake.
“Najua mnacheka kwa sababu mnajua ni kweli. Lakini mimi si mtu wa kuburuzwa usiku wa leo. Nampenda mke wangu, familia yangu, na jioni zangu. Msinitese.”
Wakati wapiga picha hao walipoanza kuondoka huku wakiendelea kurekodi, Bieber aliwaka tena:
“Hamuelewi? Siwahusu, hata kama mko kwenye barabara ya umma. Mimi ni binadamu, na nyinyi mnasimama karibu na gari langu kama kwamba mimi ni mnyama!”
Alimaliza kwa kusema:
“Acheni kunisumbua. Mnachoma moyo. Niacheni kwa amani. Asanteni.