Msanii chipukizi mwenye kipaji cha kipekee, JD Young, ambaye kwa sasa anaishi ughaibuni, ameendelea kupeperusha bendera ya Rwanda kimataifa kupitia muziki wake. Safari hii, ameachia rasmi wimbo mpya uitwao “Darling”, ambao una vionjo murua vya Afrobeat, miondoko inayoshika kasi barani Afrika na duniani kote.
Wimbo huu una mvuto wa aina yake, ukiwa umebeba ujumbe wa mapenzi uliowekwa kwenye midundo ya kuvutia inayoweza kumvutia msikilizaji wa rika lolote. JD Young ameonyesha ukomavu wa kiusanii, sauti maridhawa na utunzi wa hali ya juu – mambo ambayo yanazidi kumtambulisha kama msanii wa kimataifa anayechipukia kwa kasi.
Kwa mashabiki wa Afrobeat na wale wanaopenda muziki wa kimapenzi wenye vionjo vya Kiafrika, “Darling” ni wimbo usiopaswa kukosa kwenye playlist yako.
Tazama “Darling” kwenye YouTube na platform nyingine za muziki.