Diamond Platnumz Aandika Historia Mpya Royal Albert Hall, London – Usiku wa Bongo Fleva Uliotikisa Dunia!

Juni 13, 2025 – Historia iliandikwa jijini London! Msanii maarufu wa Tanzania, Diamond Platnumz, ameweka rekodi mpya kwa kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuitikisa Royal Albert Hall – ukumbi maarufu na wa kifahari kabisa duniani.

Kwa show iliyokuwa imepangwa kwa ubora wa hali ya juu, Diamond Platnumz aliuza tiketi zote (sold out) na kuwapa mashabiki onyesho la burudani ya kiwango cha kimataifa ambalo halitasahaulika.

Diamond alipanda jukwaani na kutoa burudani ya hali ya juu, akitumbuiza vibao vyake Kila wimbo ulipokewa kwa shangwe na nishati kali kutoka kwa mashabiki waliokuwa wakiimba naye kwa sauti moja.

Show hii haikuwa ya Diamond peke yake — alihakikisha anashirikiana na mastaa wengine wa Afrika kuifanya usiku huo kuwa wa kipekee:

Jux (Tanzania) Alitumbuiza kwa hisia kali na sauti yake laini kwenye nyimbo kama Enjoy ,

Tiwa Savage (Nigeria)Aliwasha moto wa kike jukwaani,Patoranking (Nigeria)Alichanganya reggae, dancehall na afrobeat Mr. Flavour (Nigeria) Alikuja na upako wa kiafrika walifanya mashabiki wasimame wacheze bila kukaa chini!

Instagram, TikTok, na X (Twitter) zililipuka. Video za mashabiki wakiimba kwa sauti moja, wakilia kwa furaha, na wakicheza nyimbo za Diamond zilisambaa kwa kasi.na pongezi za watu mbali mbali.

Tukio hili limeonesha wazi kuwa Bongo Fleva si muziki wa mitaa tu – ni muziki wa dunia. Diamond Platnumz ameweka alama ya kudumu kwenye historia ya muziki wa kimataifa, na amewafungulia njia wasanii wengine wa Afrika Mashariki kuota zaidi, kufanya kazi kwa bidii, na kufika mbali.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii