ZIFF 2025 YAJA KWA KISHINDO: TAMASHA LA FILAMU LENYE LADHA YA DUNIA NZIMA!

Kutoka kushoto; Mkurugenzi wa Goethe-Institute Tanzania Bw. Mpangi Otte, Mtendaji Mkuu   ZIFF Joseph Mwale, Mkurugenzi wa ZIFF, Hatibu Madudu na Mwakilishi wa Bodi Wakurugenzi, wakionesha nembo itakayotumika katika maonesho ya ZIFF mwaka huu.


Zanzibar inajiandaa kuvuma kwa shamrashamra za burudani, sanaa na utamaduni kupitia Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF) ambalo linarejea kwa kishindo mwaka huu! Kufuatia Uzinduzi  rasmi ambao umefanyika mapema leo hii June 13,2025 jijini Dar es salaam.Tamasha la ZIFF linatarajiwa Kuanza Juni 25 hadi 29, 2025, jiji la kihistoria la Ngome Kongwe litaangazwa kwa taa, sauti, filamu na vicheko kutoka kila pembe ya dunia.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Tumaini Linalochipukia” – ujumbe mzito unaoendana na wakati huu ambapo dunia inasaka matumaini mapya kupitia sanaa.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa ZIFF, Joseph Mwale, maandalizi yamekamilika rasmi na ratiba kamili ya filamu tayari ipo. Filamu Siyo Tu Burudani Lakini Inabeba Stori Inatukumbusha Hata Kwenye Giza Tumaini Linatafuta Nafasi Ya Kukua. Kwa Mwaka Huu Kila Filamu Utayoona Ni Mbegu Zilizopandwa Na Watengenezaji Filamu Waliojaribu Kuamini Kwamba Stori Zinaweza Kuchipusha Mizizi Kwenye Mioyo, Napenda Kuwakaribisha Wote Kwenye Hili Tukio, "Amesema Mwale

Na kwa wanaopenda takwimu, mwaka huu filamu 430 kutoka zaidi ya nchi 100 zimewasilishwa!

 Kutoka Afrika Mashariki pekee, filamu 174 zimepokelewa:

         •       Kenya – 54

         •       Uganda – 52

         •       Tanzania – 49

         •       Somalia – 8

         •       Rwanda – 6

         •       DR Congo – 4

         •       Burundi – 1

Na si hizo tu! ZIFF inakuwa kama Kombe la Dunia la filamu  nchi nyingine ambazo zimeongoza kuwasilisha kazi kwa wingi mwaka huu ni Iran

(79), Afrika Kusini(20), Egypt (36) huku akisema yapo na mataifa mengine mengi zaidi ya 100 kama India, China, Ufaransa, Uturuki, Nigeria, Japan na nyinginezo.

Kati ya kazi za wasanii nchini zilizoingia kwenye kinyang'anyiro ni Jenina ya Emmanuel Gembe, My Son ya Ramar King na Isarito Mwakalindile, Jacobs Daughter ya Leah Mwendamseke (Lamata), Jivu (Mustapha Machupa), Kombolela (Mustapha Machupa) na nyinginezo.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii