Tottenham Hotspur imemtangaza kocha Thomas Frank kuwa meneja wake mkuu kuchukua mikoba ya Age Postecoglou aliyetimuliwa hivi karibuni baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa taji la Europa League.
Frank ambaye alikuwa anainoa Brentford, anajiunga na Spurs kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kukubali ofa aliyowekewa mezani.
Kwa Thomas wamemteua miongoni mwa makocha wakuu wabunifu na wanaopiga sana hatua kwenye mechi.
Kutokana na rekodi isiyoacha shaka katika kuendeleza mchezaji na kikosi na wanatazamia kuiongoza timu wakati wanajiandaa na msimu ulio mbele
Mkurugenzi wa soka wa Brentford, Phil Giles ametoa shukrani kwa Frank kwa mchango alioipa klabu hiyo ambayo aliipandisha daraja 2021.