Kwa mara ya kwanza katika historia ya mpira wa Tanzania inaenda kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania NBC kwenda kuamuliwa na Waamuzi kutoka nje ya Tanzania.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF na bodi ya ligi wametangaza Waamuzi wa mchezo huo namba 184 wa Derby kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC utakaofanyika Juni 25, 2025 Kwenye dimba la Benjamin Mkapa.
Mwamuzi wa kati wa mchezo huo ni Amin Mohamed Amin Omar, akisaidiwa na Mahmoud Ahmed pamoja na Samir Gamal, huku fourth Official akiwa ni Ahmed Mahrous wote kutokea Misri huku Referee Assessor akiwa ni Ali Ahmed kutoka Somalia.