Zoezi la kutafuta meli iliyotoweka kati ya Madagascar na Comoro linaendelea

Wiki moja baada ya kutoweka kwa meli, ambayo ilitakiwa kusafiri kutoka bandari ya Majunga, Madagascar, hadi Mutsamudu, mji mkuu wa kisiwa cha Comoro cha Anjouan, waokoaji bado wanajaribu kutafuta manusura kati ya watu 30 waliokuwa ndani ya meli hiyo. Wakati ndege ya pili kutoka Madagascar ikitarajiwa kama msaada mwingine, operesheni hiyo inakusanya uwez mkuwa kutoka katika kanda nzima.

Kama zoezi la utafutaji likiendelea katika Visiwa vya Comoro kuwatafuta watu wanaowezekana kuwa walinusurika katika ajali ya meli Azfardath & Windio, iliyotoweka kwa wiki moja kati ya Madagascar na visiwa hivyo, matumaini yameanza kufifia. Meli hiyo iliyoondoka katika bandari ya Madagascar ya Majunga mnamo Juni 16, ilitakiwa kutia nanga Mutsamudu siku tatu baadaye na haikufika pwani ya Comoro.

Watu 30 walikuwa kwenye meli hiyo yenye urefu wa mita 23, ambayo mawasiliano nayo yalipotea haraka: wafanyakazi 11 na abiria 19—wengi wao wakiwa raia wa Madagascar, lakini pia raia wanne wa Comoro na raia mmoja wa Afghanistan.

Mara tu tahadhari hiyo ilipotolewa, operesheni kubwa ya utafutaji ilianzishwa, ikihusisha walinzi wa pwani ya Comoro na askari, pamoja na mamlaka ya baharini kutoka Madagascar na eneo lote. Kwa kuwa hawajapata alama yoyote ya meli hiyo au manusura wowote kufikia sasa, timu za uokoaji zinapanua eneo la utafutaji kila siku, baharini na angani. Ndege ya pili kutoka Madagascar pia inatarajiwa kuimarisha usaidizi, kulingana na Waziri wa Uchukuzi wa Comoro, Yasmine Hassane Alfeine.

Kulingana na walinzi wa pwani wa Comoro, hali ya hewa ilikuwa shwari wakatimeli ya Azfardath & Windio ilipoanza safari. Wakati meli hiyo ilikuwa na injini mbili, nadharia kadhaa za kiufundi zimewekwa mbele ili kuelezea kutoweka kwake: upakiaji mwingi, au hata kupinduka, lakini hakuna moja kati ya hoja hizi ambayo imethibitishwa. Mamlaka inapendelea kuwa angalifu na kusisitiza tena kwamba "kipaumbele ni kupata meli hiyo," kwa maneno ya Yasmine Hassane Alfeine.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii