Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameapa kwamba nchi yake haitoonyesha huruma kwa watawala wa Israel.
Matamshi hayo yanakuja saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump, kuitaka Iran kujisalimisha bila masharti.
Katika chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii wa X, Khamenei amesema lazima watoe jibu kali kwa utawala wa kigaidi wa Kizayuni.
Utakumbuka hivi karibuni Rais Trump aliitaka Iran kujisalimisha bila masharti na akajigamba kwamba Marekani inaweza kumuua Khamenei kwa urahisi.
Naye Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Ali Bahreini, amesema Israel inayalenga maeneo ya makaazi ya raia bila kutoa tahadhari huku akieleza kuwa Iran itaijibu Israel kwa mashambulizi makali na bila kizuizi.
Tutajibu kwa nguvu na tutazuia uchokozi kutoka upande wowote, iwe Israel au Marekani. Na tumetoa ujumbe kwa Marekani kwamba tutajibu vikali sana na tutazuia uchokozi wa mtu yeyote, ikiwemo Marekani hivyo kitendo kinachofanywa na Israel ni cha uchokozi.